Independent Television Ltd
Mtoto aliyeonyesha mapenzi kwa mchezaji wa Yanga Donald Ngoma, akabidhiwa jezi.

Mwandishi wa kituo cha  ITV mkoa wa Lindi,Fatuma Maumba, amekabidhi jezi yenye jina la mchezaji wa Timu ya Yanga Donald Ngoma kwa mtoto Juma Bakari,mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Mkwaya,baada ya kukutwa na mwandishi huyo akiwa amevaa fulana lake huku mgongoni akiwa amechora kwa wino wa kalamu jina la mchezaji huyo wa Yanga.

Akikabidhi jezi hiyo kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Newala,Musa Chimaye, ambaye aliona picha ya mtoto huyo kwenye mitandao ya kijamii akiwa amevaa fulana iliyochorwa kwa wino wa kalamu ndipo alipotoa fedha kwa mwandishi huyo ili ikanunuliwe jezi ya mchezaji Donald Ngoma apewe mtoto huyo kwa jinsi alivyoonyesha mapenzi makubwa kwa mchezaji huyo wa timu ya Yanga.
 
ITV ifikia katika shule ya msingi ya mkwaya,shule ambayo anasoma mtoto Juma Bakari na kukutana na walimu wake na hapa wanaelezea juu ya kuwaendeleza watoto wenye vipaji.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather