Independent Television Ltd
Jambazi auawa na wananchi akiwatoroka polisi mkoani Songwe.

Jambazi mmoja ameuawa na wananchi wakati akiwatoroka askari baada ya kubainika kufanya jaribio la  kufanya uhalifu katika mradi wa ujenzi wa kituo cha pamoja cha forodha  OSBP Tunduma mkoani Songwe ambapo jeshi  la polisi limedai kuwa jambazi huyo alivaa sare za wakandarasi na kutumia mwanya huo kutaka kutekeleza azma yake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi kamishna msaidizi wa polisi mkoa wa Songwe amesema tarehe 10 usiku wa kuamkia jumatano hii majambazi hao walipanga kufanya tukio la uhalifu katika mradi wa ujenzi wa kituo cha forodha OSBP Tunduma na kwamba baada ya kugundulika walikimbia na kutelekeza bunduki yenye  risasi 30, na zana zingine walizokuwa nazo.
 
Kamanda  Nyange  amesema  majambazi wawili walifanikiwa kutoroka wakati mmoja aliyetajwa kwa jina la Isha Martin Mwampulo (20) mkazi wa Lwasho kata ya Ndalambo wilayani Momba akinaswa na wananchi, ambapo hata hivyo baada ya kushambuliwa alijeruhiwa vibaya na kufariki dunia  akiwa njiani kuwahishwa hospitali.
 
Wakazi wa mji wa Tunduma mbali ya kupongeza jitihada za jeshi la polisi, wamesema wako tayari kushiriki kikamilifu katika kufichua wahalifu lakini wakataja kasoro ya askari kuchelewa kufika  pindi wanapoarifiwa kuhusu uhalifu jambo linalowakatisha tamaa wananchi katika kushiriki kupambana na uhalifu.
 
Kamanda nyange ameendelea kutahadharisha kuwa mkoa wa songwe sio mahali salama kwa wahalifu na kupongeza ushirikiano wa wananchi kwa jeshi la polisi hadi hivi sasa.
 
 
 
 
 
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather