Independent Television Ltd
Ujenzi holela wa makazi ni kikwazo kwa Jeshi la Zimamoto kufikia malengo Ruvuma.

Kufuatia kukithiri kwa matukio ya majanga ya moto mkoani Ruvuma,mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dokta Binilith Saatano Mahenge ameziagiza halmashauri za wilaya kupitia idara za ardhi na mipango miji mkoani humo kuanzia sasa kutopitisha ramani na michoro ya majenzi hadi zipate kibali toka Jeshi la Zimamoto na uokoaji ili kuondokana na ujenzi holela wa makazi usiozingatia uwepo wa miundombinu ya barabara na maji pindi majanga ya moto yanapojitokeza.

Agizo hilo amelitoa wakati jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani hapa lilipokuwa linatoa elimu ya uokozi juu ya majanga ya moto na mengineyo.
 
Nae Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Ruvuma,Eria Kakwembe akiwa katika viwanja vya matarawe mjini Songea,wakati wa uzinduzi wa namba ya dharura ya 114 juu ya utoaji taarifa za majanga ya moto pindi yanapotokea amewataka wananchi kutumia fursa ya namba hiyo ili kuepusha madhara zaidi ya majanga ya moto na mengineyo.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather