Independent Television Ltd
Polisi Simiyu wamekamata malori 5 ya mizigo yaliopakia abiria kinyume cha sheria.

Jeshi la polisi mkoani Simiyu limefanikiwa kukamata magari matano aina ya malori yaendayo minadani pamoja na abria 18 waliokutwa wamepanda malori hayo kinyume cha sheria.

Siku chache baada ya mkuu wa kikosi cha usalama barababarani nchini,Fotunatus Musilimu kupiga marufuku magari yote makubwa aina ya malori yanayokwenda mnadani kubeba abiria,Jeshi la polisi mkoani Simiyu limekamata magari makubwa matano yanayoenda minadani yakiwa yamebeba zaidi ya abiria 18 wakiwa wamepakiwa ndani ya maroli hayo pamoja na mizigo wakielekea minadani.
 
Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Simiyu Kamishina Msaidizi wa polisi Boneventure Mushongi amesema wananchi hao wamekamatwa majira ya saa 9 usiku katika katika barabara ya Bariadi –Itilima baada ya polisi kuwawekea mtego.
 
Katika hatua nyingine Kamanda Mushongi amesema Jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata vitu mbalimbali ikiwemo nyara mbalimbali za serikali pamoja na watuhumiwa watano pikipiki zinazotumika kufanya uwindaji haramu ndani ya hifadhi ya Serengeti na Pori la Akiba Maswa,pombe haramu ya gongo,madawa ya kulevya aina ya mirungi na nyavu haramu za kuvulia samaki ndani ya Ziwa Victoria kufuatia misako inayoendelea mkoani hapa ambapo watuhumiwa waliokamatwa katika makosa hayo wamefikishwa mahakamani.
 
Kufuatia matukio hayo Kamanda Mushongi ametoa wito kwa wananchi wote kuendelea kufanya kazi zao halali ipasavyo na kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwani jeshi hilo linaendelea na msako ambao hauna kikomo ili kuhakikisha wananchi wanaishi salama.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather