Independent Television Ltd
Kalemani atangaza kiama kwa watumishi TANESCO na vishoka watakao kushirikiana na wateja kuiba umeme.
Waziri wa Nishati na Madini Dkt.Medard Kalemani ametangaza kiama kwa watumishi wote wa TANESCO na vishoka watakao bainika kushirikiana na wateja kuiba umeme huku akielezea mikakati yake kuhakikisha umeme unakua wa uhakika.
 
Waziri Kalemani ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipikua akizungumza na maafisa wa shirika hilo ambapo amesema shirika limekuwa likipoteza mapato mengi kufuatia umeme unaopotea kutokana na wizi unaofanywa na baadhi ya wateja.
 
Rai hiyo imetokana na operesheni inayofanywa na TANESCO ambayo imeanzia jijini Dar es Salaam ambayo wateja zaidi ya mia moja wamebainika kutumia umeme bila kulipia hali inayotia hasara shirika. 
 
Katika operesheni hiyo baadhi ya wateja wamekua wakizikimbia nyumba zao kama Kamera ya  ITV ilivyo wanasa na kufanikiwa kuzungumza na baadhi ya wapangaji.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather