Independent Television Ltd
Moto wateketeza kituo cha yatima Monduli.

(Picha na Maktaba yetu)

Watu kadhaa wakiwemo watoto wamenusurika kifo baada ya moto kuwaka na kuteketeza zaidi ya gunia sitini za Mahindi ya chakula mashine tatu za kusaga na kukobo nafaka pamoja na vifaa vingine katika kutuo cha kulelea watoto yatima na wazee wasiyojiweza cha amana Chidren home kilichopo kata ya Esirarei wilaya ya Monduli.

Mlezi wa kituo hicho cha kulelea watoto cha amana Chridren home Steven kimbi anasema tukio hilo limetokea majira ya saa tano usiku wamejitahidi kuuzima lakini ilichukua muda mrefu kwakuwa walikuwa wanatumia maji ya kuchota kwa ndoo hivyo chakula kilichowemo kwenye ghala chote kimeteketea mashine za kuzaga za kituo zimeteketea na hakuna mtu alipata madhara kwenye tukio hilo.
 
Wahudumu wanaishi ndani ya kituo hicho wakaeleza mazingira ya moto huo ulivvyotokea na kwamba umesababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni themanini.
 
Baadhi ya viongozi wa mtaa uliyotokea tukio ilo wameomba wasamariwema kujitolea kuwasaidia wazee na watoto wanaolelewa kituo kituoni hapo.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Wakulima kulazimishwa kuuza korosho kinyume na bei elekezi. Je ni utawala bora?
Ndio
Hapana
Vote Now
Results
Weather