Independent Television Ltd
TAKUKURU yatoa onyo kwa watendaji wa serikali.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU imetoa onyo kwa watendaji waliopewa dhamana na serikali kuacha kutumia nafasi zao vibaya kwa kujipatia  vipato nje ya malipo wanayolipwa na serikali  kwani kwa kufanya hivyo hatua kazi za sheria zitachukuliwa dhidi yao.
 
Onyo hilo dhidi ya watendaji wa serikali limetolewa Dar es Salaam na naibu mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU wakati akitangaza donge nono la milioni kumi kwa raia akakayefanikisha kupatikana  kwa  aliyekuwa mhasibu wa taasisi hiyo Bw. Godfrey Gugai ambaye alikutwa akimiliki nyumba 7,viwanja 33,na  magari 6 mali zinazotajwa kuwa ghali zaidi ukilinganisha na mshahara wake.
 
Naibu mkurugenzi huyo amesema kwa sasa serikali iko katika mapambano makali dhidi ya rushwa na kwamba haitasita kumchulia hatua yeyote atakayebainika kutumia nafasi aliyonayo serikali kwa kujinufasha binafsi na kusema si kosa kwa mtumishi wa serikali kuwa na mali  na kwamba jambo la msingi ni namna gani mtumishi huyo amepata mali hizo.
 
Mapema mei 8 mwaka huu TAKUKURU ilitoa waraka unaoonyesha mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam ilikwisha kutoa zuio la mali zote za Bw. Godfrey Gugai ambaye anakabiliwa na makosa ya rushwa au yanayofafana na rushwa  ikiwa ni kufuatia ombi la mkurugenzi wa mashitaka DPP chini ya kifungu cha 38 1 a na b  cha sheria ya kuizia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 katika shauri namba 13 la 2017
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather