Independent Television Ltd
Wanafunzi 21 St. Paul wilayani Nyasa wanashikiliwa na polisi kwa uhalifu.

Wanafunzi 21 wa kidato cha tano na sita shule ya sekondari ya St. Paul Liuli wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kufanya uhalifu kwa kuharibu miundombinu ya shule kwa kupasua vioo vya madirisha, kukutwa na bangi, nondo pamoja na silaha zenye ncha kali zikiwemo visu na mapanga.

 Wanafunzi hao ambao waliungana kufanya uhalifu huo majira ya saa tatu za usiku, walianza kwa kuzima mifumo ya umeme shuleni hapo na kisha kufanya uvamizi wa kupasua vioo vya madirisha ya shule pamoja na kupiga mawe.
 
 
Mmoja wa walimu wa shule hiyo, Bw. Mosses Mwaitandaje amesema chanzo cha wanafunzi hao kufanya uhalifu huo ni baada ya mwanafunzi mmoja wa kidato cha sita, Justine Mlekoni ambaye alisimamishwa shule kwa kosa la kukutwa na simu ya mkononi maeneo ya shule kinyume cha utaratibu kudai arejeshewe simu yake kinguvu kutoka kwa makamu mkuu wa shule Bw. Doodluck Essau.
 
 
Mkuu wa wilaya ya Nyasa, Bi. Isabela Chilumba ametembelea na kukagua uharibifu uliofanywa na wanafunzi hao katika shule hiyo, hata hivyo kamati ya ulinzi na usalama ilivyokagua bweni la wanafunzi hao walikuta wakiwa na silaha zenye ncha kali ikiwemo visu, mapanga, nondo, karata pamoja na bangi huku akiagiza bodi ya shule ichukue hatua kali dhidi yao.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather