Independent Television Ltd
Wakulima wameshauriwa fedha wanazozipata kwa kuuza Korosho wakafanyie mambo ya maelendeo.

Makamu Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika Runali, Saidi Abdallah Kalindima,amewashauri wakulima wa Korosho katika wilaya ya Ruangwa, Nachingwea na Liwale, kuwa fedha wanazozipata baada ya kuuza Korosho zao wazitumie kwa ajili ya kufanya mambo mbalimbali ya  maendeleo kama vile  kujenga nyumba bora, kuandaa mashamba pamoja  na kuwasomesha watoto wao kwa maana ya kuwanunulia vifaa vyote vya shule.

Ushauri  huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika Runali, wakati akizungumza na wananchi pamoja na wakulima wa zao la korosho katika kijiji cha Matambarale, wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather