Independent Television Ltd
Madereva tisa wa magari ya abiria wafungiwa leseni kwa kusababisha ajali na vifo mkoa wa Ruvuma.

Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Ruvuma kimewafungia leseni madereva tisa wa magari ya abiria waliosababisha ajali na kusababisha vifo vya watu na majeruhi ikiwa ni mikakati ya kikosi hicho mkoani Ruvuma  kupunguza ajali.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani  mkoa  Ruvuma uliofanyika katika  kituo cha mabasi ya Mbinga, Kaimu Mkuu wa kikosi hicho mkoa wa Ruvuma   ADAM KIMBESI amesema  polisi wanalazimika kufanya hivyo ili kupunguza ajali.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya  Usalama Bara barani mkoa wa Ruvuma Bwana  PHILIP SHANTEMBO ametaka uwepo ushirikiano kati ya polisi ,abiria na madereva ili kupunguza  ajali na kwamba kila mmoja atimize wajibu wake.
 
Mkuu wa wilaya ya Mbinga Bwana COSMAS NSHENYE amewataka polisi kuendelea kusimamia sheria na wao pia kuwa wa kwanza kufuata sheria.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather