Independent Television Ltd
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh.Freeman Mbowe awaasa wananchi wasiruhusu vyama vya siasa kujenga ufa miongini mwaomkoani Mtwara.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Mheshimiwa FREEMAN MBOWE amewaasa wananchi wa kata ya Chanika Nguo wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wasiruhusu vyama vya siasa kujenga ufa miongini mwao bali viwe sehemu ya kuwapa fursa mbadala ya kupingana kwa hoja na si uadui.

Ametoa hadhari hiyo wakati akimnadi mgombea  udiwani wa chama hicho  JAMES KAOMBE katika kata hiyo.
 
Kwa upadne wake, mgombea wa kiti hicho Bwana JAMES KAOMBE amewaomba wananchi wa kata hiyo kumpa kura za ndiyo ili aweze kuunganisha juhudi zao za kujiletea maendeleo huku Mbunge wa jimbo la Ndanda Mheshimiwa CECIL MWAMBE  akiwataka wananchi hao wasifanye makosa bali wamchague mgombea huyo .
 
Katika kampeni hizo Mheshimiwa mbowe amewapokea wanachama wapya mia tatu waliohama kutoka Chama Cha Mapinduzi.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather