Independent Television Ltd
Wafanyakazi wa kiwanda cha Nguo cha 21st Century kilichopo mkoani Morogoro wagoma kwa mara ya pili.

Wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha 21st century kilichopo Kihonda manispaa ya Morogoro, wa kitengo cha ushonaji wamerudi kwenye mgomo kwa mara nyingine, wakiendelea kushinikiza kuondolewa kwa meneja wa kitengo hicho, ambaye wanadai amekuwa akiwafanyia vitendo vya unyanyasaji hususani kuwatolea maneno ya kashfa, huku baadhi ya wafanyakazi kitengo cha umaliziaji nao wakiunga mkono mgomo huo kwa lengo la kutaka kuongezwa mshahara.

 Wakizungumza kwa jazba wakiwa kiwandani hapa wafanyakazi waliogoma wamesema kamwe hawawezi kuendelea na kazi endapo uongozi huo hautabadilishwa na kuongezwa mishahara kwakuwa kazi wanazofanya ni ngumu tofauti na kiasi wanacho lipwa.
 
Aidha kwa upande wa wafanyakazi kitengo cha umaliziaji wamesema tatizo hilo la mishahara mshahara mdogo nilasiku nyingi lakini walikuwa wanashindwa kuchukua hatua kulingana na uongozi uliokuwepo ambapo wameomba serikali kuingilia kati.
 
Nao uongozi wa kiwanda hicho umesema wataongeza mshahara kwa asilimia 7 kuanzia mwezi huu na kuhusu malalamiko mengine mkurugenzi raslimali watu hassan dewji ameahidi kuyafanyia kazi.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather