Independent Television Ltd
Wakulima Mvumi wataka ufafanuzi kuhusu kukamatwa kwa wenzao zaidi ya 40.

Wakulima wa kijiji cha Mvumi wilayani kilosa mkoani Morogoro wameitaka serikali kuwafafanulia kilichosababisha wenzao zaidi ya 40 kukamatwa na polisi wakati wakiandaa  mashamba yao kwa shughuli za kilimo ambayo wana hatimiliki ya kuyamiliki kisheria.

Wakulima hao wamesema hayo baada ya kurejeshewa hekari 2,500 zilizoshindwa kuendelezwa na mwekezaji,ambazo kati yake,halmashauri ya wilaya ya Kilosa iligawa hekari 1000 kwa vijiji vya Mvumi na Gongwe na kwamba baada ya kauli ya wilaya kutaka wenye hati za mashamba wasijumuishwe katika mgao wa eneo lililotolewa,kamata kamata ya waliokuwa wanaandaa mashamba ikafanywa na polisi.
 
Alipohojiwa kuhusu tukio hilo,Mkurugenzi Mendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilosa, Kessy Mkambala, amesema kilichofanyika ni kuchukua hatua kivitendo kwa  wasiotaka kufuata taratibu huku mkuu wa wilaya hiyo adam mgoyi akisema ardhi hiyo sio mali ya wakulima wa Mvumi.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather