Independent Television Ltd
Wahabeshi 16 na Mawakala wanne watiwa mbaroni.

 

Kikosi kazi cha Maafisa Uhamiaji mkoani Tanga kimewakamata wahamiaji haramu 16 kutoka Ethiopia pamoja na mawakala wanne raia wa Tanzania wanaojihusisha na bishara ya kuwasafirisha kwenda Afrika ya Kusini,wametiwa mbaroni na mkoa wa Tanga kwa kosa la kukiuka sheria za nchi.
 
Akizungumza mara baada ya makundi ya wahamiaji hao kukamatwa katika kijiji cha Mnzavar kilichopo mpakani mwa Kenya na Tanzania,Afisa uhamiaji mkoa wa Tanga Naibu Kamishna wa uhamiaji Cyprian Ngonyani amesema kikosi kazi walichokiunda katika eneo la Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania linatokana na agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli kuwaagiza maafisa hao kuhakikisha mipaka inadhibitiwa ili kuzuia uingiaji wa wahamiaji haramu.
 
Mmoja kati ya mawakala aliyetiwa mbaroni na idara ya uhamiaji mkoa wa Tanga Philip Francis amesema wao wanatumiwa fedha na mawakala wenzao wenzao waliopo nchini jirani ya Kenya kisha wanafanya mchakato wa kuwatorosha kwenda mikoa ya Kusini ma Tanzania.
 
kufuatia hatua hiyo Afisa Mdhibiti wa idara ya uhamiaji mkoa wa Tanga,Daniel Gullum amesema ongezeko la wahamiaji haramu kukamatwa katika wilaya ya Mkinga linatokana na kuwepo kwa njia za panya hasa eneo la Kenya ambazo zimekua zikitumiwa kwa ajili ya kuwasafirisha lakini kikosi kazi kilichoanzishwa kimeanza zoezi la kudhibiti.
 
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather