Independent Television Ltd
Makamu wa Rais amehimiza ujenzi wa vituo vya afya uzinagatie uwepo wa wodi ya mama na mtoto.
Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu amehimiza ujenzi wa vituo vya afya uzinagatie uwepo wa wodi ya mama na mtoto ili kukabiliana na tatizo la vifo vya wananwake na wajawazito hapa nchini.
 
Makamu wa Rais amesema hayo mjini Iringa kwenye kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku tano mkoani Iringa huku akiagiza ufuatiliaji wa takwimu za vifo vya wanawake wajawazito hadi maeneo yasiyofikika ili serikali iweze kufahamu hali halisi ya tatizo hilo.
 
Ameupongeza mkoa wa Iringa kwa mafanikio makubwa ya kupunguza vifo vya mama na mtoto lakini akataka jitihada zaidi ziongezwe ili kukomesha kabisa tatizo hilo lakini ameshitushwa na ongezeko la takiwimu za maambukizi ya virusi vya ukimwi.
 
Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi na watendaji wa serikali wakiwemo viongozi wa dini ambapo Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania Tarcisius Ngalalekumtwa amewaomba wataalamu wasaidie wananchi jinsi ya kuboresha shughuli zao ili kupunguza umasikini wa kipato.
 
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather