Independent Television Ltd
Lukuvi apiga marufuku wathamini wa serikali kufanya miradi nje ya serikali.

Waziri wa Ardhi Nyumba na makazi William Lukuvi amepiga marufuku wathamini wa serikali kufanya tathmini nje ya miradi ya serikali na kuitaka bodi ya usajili wa wathamini kufanya kazi kwa ufanisi ili kumaliza dosari nyingi zinazojitokeza katika taaluma hiyo.

Waziri Lukuvi ametoa agizo hilo wakati akizindua bodi mpya ya usajili wa wathamini ambapo ameitaka kuhakikisha wanawachukulia hatua  wanadhibiti na kumaliza tatizo la wa thamani.
 
Aidha Waziri Lukuvi amesema mpango wa serikali ni kuhakikisha kabla ya mwezi wa tatu wanateua wathamini wakuu wasaidizi katika kanda ili kazi zote za uthamini ziishie katika ngazi ya kanda.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather