Mkurugenzi wa Biashara na Ugavi wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero, Bw. Fimbo Butallah amesema maonesho ya NaneNane yanaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuonesha teknolojia za kisasa za kilimo, kuimarisha ushirikiano wa sekta, na kufungua fursa mpya kwa wadau katika mnyororo wa thamani.