Independent Television Ltd
'ITV TANZANIA APP'
ITV imezindua mfumo mpya maarufu ‘itv popote’ mfumo huu unakuwezesha kuangalia itv na capital tv popote pale ulipo ulimwenguni, kupitia simu yako ya kiganjani.
 
Mfumo huu unafanya kazi kwenye simu za kupangusa (smart phones).
Jinsi ya kupata huduma hii.
 
Kama wewe unatumia simu yenye mfumo wa android,’itv tanzania app’inapatikana PLAY STORE
Kama wewe unatumia simu yenye mfumo wa IOS(IPhones) “ITV TANZANIA APP’ INAPATIKANA APPLE STORE.
 
Mfumo huu umeanza vizuri unakua kwa kasi na umepokelewa vizuri sana, hivyo umetengeneza fursa kwa wewe mtanzania kutangaza biashara yako kupitia mfumo huu ambao unawafikia mamilioni ya watumiaji wa simuza mkononi.
 
Lakini pia ITV inatoa fursa kwa wale wote wenye sifa na uwezo wa kuwa mawakala wa kufanya mauzo ya matangazo ya biashara kupitia mfumo huu.
 
Mawakala wawe na sifa zifuatazo:
 
  • Wawe na kampuni iliyosajiliwa na mamlaka husika.
  •  
  • Wawe na kibali cha kufanya biashara na leseni kutoka tra na mamlaka husika
  • Wawe na ofisi inayofahamika.
  •  
  • Ofisi iwe na kompyuta au kipakatalishi (laptop).
  •  
  • Wawe na barua ya utambulisho toka serikali za mitaa
  •  
Wenye nia na sifa tajwa hapo juu wawasiliane nasi kupitia barua pepe [email protected]
Au anaweza kupiga simu hizi kwa maelezo zaidi: 0767 777147, 0682 951525, 
 
ITV POPOTE, FURAHIA MAISHA.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather