Back to top

"RAIS DK.SAMIA AMEFANYA MAGEUZI SEKTA YA AFYA" - MOLLEL

28 April 2024
Share

Naibu Waziri wa Afya, Dkt.Godwin Mollel, amesema Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya kwa kuwekeza kwenye teknolojia, elimu, wataalamu, kupeleka huduma karibu na wananchi pamoja na ununuzi wa vifaa tiba vya uchunguzi.
.
Mollel ameyasema hayo, mkoani Tabora, alipomuwakilisha Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Dotto Biteko, katika Maadhimisho ya kilele cha miaka 25 ya huduma ya maendeleo ya mtoto na kijana nchini, ambapo ameeleza kuwa  wengi walikuwa wakipelekwa India kwenda kutibiwa kwa fedha nyingi lakini kwa sasa huduma hizo zinapatikana hapa nchini.
.
Amesema ilikuwa ukienda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili miaka minne iliyopita ukiwa una tatizo la moyo unafunguliwa kifua kizima, lakini kwa sasa zaidi ya bilioni 28 zimetolewa kwa ajili ya kununua vifaa tiba ambapo mgonjwa anaingizwa katika mashine na hakuna haja ya kufungua kifua na baada ya muda mfupi anaruhusiwa kurudi nyumbani.