Independent Television Ltd
TFF yasimamisha mchakato wa uchaguzi Simba.

 Shirikisho la soka tanzania TFF limesimamisha mara moja mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Simba hadi hapo kamati ya utendaji ya Simba itakapo unda kamati ya maadali.

Akizungumza na waandishi wa habari rais wa TFF Jamal Malinzi amesema TFF imepokea malalamiko kadhaa juu ya ukiukwaji wa maadili wa wagombea na wanachama kadhaa wa klabu ya Simba.

Malinzi amesema kwa mujibu wa katiba ya Simba ibara ya 16 kifungu (e) na ibara ya 30 kifungu (h) kamati ya utendaji ya Simba imeagiza iunde kamati ya maadili mara moja  na kwamba kamati hiyo ya maadili ikae mara tu baada ya kuundwa na kusikiliza mashauri yote ya kimaadili ambayo kwa sasa yamewasilishwa TFF na walalamikaji kadhaa.

Aidha Malinzi amesema kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za TFF ibara ya 2 kifunga cha (4) kamati ya utendaji ya Simba itaendelea kuwa madarakani hadi hapo mchakato wa uchaguzi wa Simba.

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather