Independent Television Ltd
Simba hawana mpango wa kumrejesha Emmanuel Okwi.

 Uongozi wa timu ya simba umedai hauna mpango wa kumrejesha  mshambuliaji wake wa zamani emmanuel okwi huku ukimshangaa mchezaji huyo kuwepo jijini dar es salaam .

Simba mnyama mkali asokuwa na pupa awindapo tena asokazanisha mwendo  maarufu wekundu wa msimbazi,wenye makaazi yao mitaa yenye pilikapilika nyingi Msimbazi Dar es Salaam imethibitisha kuwa hauna niya ya kumrejesha Emanule Okwi na inasubiri tarehe 30 ya mwezi huu kujua hatma ya fedha zao kutoka kwa Etohil de sahil.

Emanuel Okwi aliyekuwa lulu kwa wanagenzi Simba aliuzwa kwa Etohil de sahil ya Tunisia ameonekana Dar es Salaam akihaha huku na huko huku timu yake ikimtafuta bila mafanikio,na bado msukuma ndinga huyo hajathibitisha kama ndoa imemshinda ama laa.

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather