Independent Television Ltd
Mrisho Ngasa amewasilisha Sh. Mil 45 alizokuwa akidaiwa na Simba.

 Hatimaye mchezaji Mrisho Ngasa amewasilisha kiasi cha shilingi milioni 45 alizokuwa akidaiwa na timu ya soka ya Simba na kumaliza rasmi adhabu yake.

 
Zile riwaya ndefu za akina Chinua Achebe,hamkani si shwari Shaaban Robert kusadikika inashabibihiana na hii.ni saa tisa alaasiri jua likianza kupoteza nguvu jijini Dar es Salaam, upepo nao ukivuma kutoka mashariki kuelekea magharibi,katika uwanda wa TFF ITV michezo ilipotegesha mitambo yake kwa muda zinaingia gari mbili na mojawapo ni gari la kukodisha yaani tax anateremka mshambulizi hatari Mrisho Ngasa akiambatana na msemaji wa Yanga Baraka Kizuguto na kiongozi mwingine mwandamizi Patrick Nagy wakiwa na begi lenye ushahidi ya hundi ya malipo halali ya shilingi milioni 45,mlipwaji ni clabu ya Simba.
 
Akionekana ni mjeruhiwa wa msongo wa mawazo na sasa anaondokana na babaiko kwakutabasamu mara kwa mara,Mrisho Ngasa ameieleza ITV michezo pekee yakuwa amelipa fedha hizo kwa jasho lake peke yake ingawa hakutenda kosa na sasa anaingia katika mapambano.
 
Safari ya Ngasa kutua mitaa hiyo ya Jangwani ilikuwa na mawimbi mengi,kwani awali aliondoka mitaa hiyo akaenda mitaa isopkuwa na muradli chamazi kwa wana Azam Fc, ndoa ikaingia shubiri akabeba mizigo na kutua mitaa yenye pilika pilika nyingi msimbazi kwa wekundu wa Msimbazi,nako hakukukalika chai ikawekwa chumvi,kabeba mizigo na kutua mitaa ya Twiga na Jangwani wanamsimbazi nao wakahamaki kaondoka kabla ya mkataba kumalizika na tena kaondoka na fedha kabatini pamoja na kukanusha vilakini Mrisho amezilipa hii leo. Hapana shakha mashambulizi kuelekezwa lango ka Ruvu Shooting kesho yataongozwa na Mrisho Ngasa.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather