Independent Television Ltd
Rais wa TFF : Lazima uchaguzi mkuu wa TFF kufunyika Oct 27,2013.

 Rais wa shirikisho la soka Tanzania -TFF Leodgar Tenga ameapa kuwa ni lazima uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo kufanyika kama ulivyopangwa Oktoba 27 licha ya baadhi ya wadau kutishia kuusimamisha kwa madai ya kutoridhika na uamuzi wa kuondolewa katika kinyang'anyiro hicho.

Rais Tenga amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa uchaguzi huo ambao awali uliingia dosari baada ya shirikisho la soka la kimataifa FIFA kuagiza kusitishwa kwa mchakato huo na kutaka kuundwa kwa kamati za maadili baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wagombea walioenguliwa.

Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika mwezi Februari mwaka huu ambapo rais Tenga amesema dhamira ya TFF ni kuona uchaguzi huo unakuwa huru na wa haki na kuongeza kuwa mchakato wa uchaguzi huo sasa unakwenda vizuri tangu FIFA ilivyoagiza kuanza upya.

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je sekta ya umma na sekta binafsi zinashirikiana kufanikisha azma hiyo
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather