Independent Television Ltd
E.A Tv na Radio wametangaza kuwaleta Psquare kufanya Onyesho Nov. 23 jijini DSM.

 East Africa televisheni na radio wametangaza rasmi kuwaleta  wanamuziki  mapacha Peter na Paul Okoye maafufu  kama Psquare kutoka Nigeria kufanya onyesho hapo Novemba 23  mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa East Africa Televisheni na radio Hillary Daudi maarufu kama Zembwela amesema  katika onesho hilo Psquare watakuja na wanamuziki 13 na watafanya tamasha la muziki la moja kwa moja yaani live band.

Katika hatua nyingine mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Kelvin Twisa amesema kampuni ya Vodacom wameamua kuwa wadhamini rasmi wa onyesho hilo ili kuleta ushindani kwa wanamuziki nchini.

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather