Independent Television Ltd
TFF imetangaza orodha ya mwisho ya wagombea wa uchaguzi wa TFF na wa bodi ya ligi-TPL

 Kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka Tanzania -TFF imetangaza orodha ya mwisho ya wagombea wa uchaguzi wa TFF na wa bodi ya ligi-TPL utakaofanyika Oktoba 25 na 27 jijini Dar es Salaam huku ikiwataka wagombea hao kutumia kipindi cha kampeni kuanika mikakati yao katika kuinua soka la Tanzania badala ya kutumia muda huo kuupaka matope uongozi unaomaliza muda wake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi hamidu Mbwezeleni amesema kampeni zimeanza rasmi leo na zinatarajia kumalizika Oktoba 24 kwa upande wa uchaguzi wa bodi ya ligi na Oktoba 26 kwa upande wa uchaguzi wa TFF na kusisitiza kuwa mgombea yoyote atakayemkashfu mwingine ataondolewa mara moja kwenye kinyang'anyiro hicho kwa mujibu wa kanuni mpya ya uchaguzi ya mwaka 2013.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Moses Kalua na mjumbe Mustapha siyami wamefafanua vigezo vilivyotumika kuwaengua baadhi ya wagombea kwenye kinyang'anyiro hicho ambacho awali kiliahirishwa na shiriksho la soka la kimataifa-FIFA kufuatia baadhi ya wagombea kulalamika kutotendewa haki katika zoezi la usaili.

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather