Independent Television Ltd
Ligi Kuu ya Vodacom, Rhino Rengers yashinda Tabora, Yanga Yashinda DSM

Ligi kuu ya Tanzania bara imeendelea tena katika uwanja wa Ally Hassani Mwinyi mkoani Tabora kwa kuzikutanisha timu za Rhino Rengers ya Tabora na timu ya JKT Ruvu.

Mchezo huo uliofanyika katika  dimba hilo timu ya Rhino inajilaumu kwa kupata nafasi kadhaa za wazi ambapo wachezaji wangejipatia magoli mengi lakini walikuwa wakiishia kupiga nje na wakati mwingine kumzawadia golikipa

Mwandishi wetu Simon Kabendera - Tabora ameiambia ITV kwamba Pamoja na mchaka mchaka huo wa majeshi hayo mawili yakikutana kuonyeshana kandanda safi katika dakika ya tisini mchezaji Abas Mohamedi alifanya kazi ya ziada na kuandika goli lililowainua mashabiki na kuiongezea timu ya Rhino pointi tatu.

Aidha katika mchezo mwingine Hapa DSM Timu ya Yanga imeendeleza vyema jitihada za kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya leo kuifunga Mgambo JKT mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  
Ushindi huo dhidi ya Mgambo iliyofungwa 7-0 na Simba SC, unaifanya Yanga SC itimize pointi 22, baada ya kucheza mechi 11, Azam FC inaongoza ligi hiyo kwa pointi zake 23 sawa na Mbeya City.
 
Hadi mapumziko, tayari Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na beki wa kimataifa wa Rwanda, mwenye asili ya DRC, Mbuyu Twite dakika ya 32Twite alifunga bao hilo kwa shuti la mbali baada ya kuanzishiwa mpira wa karibu wa adhabu na kiungo Athumani Iddi ‘Chuji’.
Yanga ilitawala zaidi mchezo kipindi hicho na kukosa mabao mengi ya wazi,lakini
Kipindi cha pili, Yanga tena walirudi na moto na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 50, mfungaji Hamisi Kiiza

Bao hilo liliwachagiza Yanga na kuendelea kushambulia kwa kasi lango la timu hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na hatimaye kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 67, mfungaji Kavumbangu.
Kavumbangu alifunga bao hilo akiunganisha krosi maridadi ya Simon Msuva, aliyeanzishiwa mpira wa kurusha wa karibu na Mrisho Ngassa.  
 

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather