Independent Television Ltd
Bonanza la TRA lafana Tabora

Wakati mamlaka ya mapato nchini (tra) ikiazimisha wiki ya mlipakodi kwa kuendesha bonanza mbali mbali, mkoani tabora mamlaka hiyo imeendesha zoezi hilo kwa kuwakutanisha mashirika kadhaa katika michezo kwa lengo la kuikutanisha jamii.

 

Akizungumza na washiriki wa bonanza hilo lililojumuisha taasisi za fedha za NMB, CRDB, VETA, benki ya posta TTCL, TCCIA  waendesha pikipiki maarufu kama boda boda, waandishi wa habari, na timu ya wanawake mkoani Tabora.

 

Meneja wa TRA Tabora Bw. Laurent amesema kuwa, malengo ya bonanza hilo ni kuwakutanisha wadau wa TRA ili kushiriki katika michezo, kubadilishana mawazo pamoja na kufahamiana.

 

Hata hivyo washiriki wa bona hilo wameuambia mtandao wa ITV kuwa bonanza kama hilo linatakiwa kufanyika kila mwezi kwani malengo ni kujenga afya, kutokana na watumishi katika mashirika kutokana kazini wamechoka na kukimbilia majumbani mwao na kulala.

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather