Independent Television Ltd
Mabadiliko ya uongozi TFF yamng'oa katibu mkuu..

Kikao cha kwanza cha Kamati mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana chini ya Rais, Jamal Emil Malinzi kimemuengua Katibu Mkuu wa kuajiriwa, Angetile Osiah Malabeja.

Rais Malinzi, alifungua kikao kwa ajenda ya kumuengua Angetile na Wajumbe wakaafiki.
Angetile amepewa likizo ya malipo mpaka hapo  atakapomaliza Mkataba wake mwezi ujao, aliyekuwa afisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura Mgoyo atakatimu nafasi yake.
 
Na hii ndio iliyokuwa taarifa kwa vyombo vya habari:
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Bw. Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Uteuzi huo ni kuanzia Novemba 2 mwaka huu.
Aidha aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.
Kamati ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika utekelezaji wa majukumu yake.
Jamal Malinzi
Rais, Dar es Salaam
Novemba 3, 2013
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto