Independent Television Ltd
Simba imeibuka na ushindi mnono wa 3 1 dhidi ya Yanga.

 Hatimaye mpambanbo wa watani wa jadi Simba na Yanga umemalizika kwa timu ya soka ya Simba kuibuka na ushindi mnono wa mabao matatu kwa moja.

Ni kwa sababu tu mahakamani ya uhalifu wa kimataifa ICC haipokei kesi za binadamu kuumizwa moyoni kwa matokeo ya soka lau kama ingelipokea tuhuma za binadamu kuumizwa kwa matokeo ya soka,basi wachezaji wa Yanga na mwalimu wao Ernei brants wangelikuwa mbele ya Fatou Binsouda wakijibu tuhuma nzito za kuwaumiza mashabiki wao roho kiasi cha kupoteza matumaini kabisa mbele ya mnyama Simba aliyeonekana kumwagiwa maji nakuigiza kama paka lakini Simba ni Simba tu hatakama amelowa.

Simba mnyama mkali,asokazanisha mauongo,hutembea kwa mapana asikazanishe maungo maarufu wekundu wa msimbazi,wazaliwa wa mwaka 1936,wenyeji wa mitaa yenye pilikapilika nyingi Msimbazi Dar es salaam imedhihirisha kuwa wao ni wababe tena majemedari mbele ya Yanga wasiyoeleweka hawafuti hawanaandiki,hiyo ni baada ya wekundu hao kuwafumua watani wao kwa mabao 3-1.

Raiya wa Burundi Hamisi Tambwe ndiye aliyeanza uchuokozi kwakufunga bao la awali katika dakika ya 14,bao la pili likifungwa tena na Hamisi Tambwe kwa mkwaju wa penalti huku bao la tatu likisukumwa wavuni na Juma Awadh,bao lakufutia machoozi kwa Yanga liliwekwa kimyani na Emmanuel Ikwi.

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Maandalizi ya timu za taifa katika mashindnao ya kimataifa. Je yamewekewa utaratibu kupata timu bora?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather