Independent Television Ltd
Timu ya soka ya Yanga imemfukuza kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Ernie Brant's

 Timu ya soka ya Yanga imemfukuza kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Ernie Brant's na timu hiyo kuwa chini ya kocha msaidizi Fredy Felex Minziro kuanzia leo.

 Visa vingine vinaweza kufananishwa na nyimbo za Sikinde ama Dar intanational, talaka ya hasira ni mbaya sana usimpe talaka subiri japo kwa mwaka japokuwa mwagombana punguza zako hasira. Uongozi wa timu ya soka ya Yanga chini ya mwenyekiti wa kamati ya mashindano Abdallah Bin Klebu leo imetoa tamko la kusitisha mkataba na mwalimu mkuu wa timu hiyo mdachi Erney Brant's kwa sababu hajafikia malengo waliyotaraji huku mwanachama John Jambele akiunga mkono uamuzi huo lakini akitaka na Juma Kaseja naye amfuate kocha huyo.

Pamoja na hayo Abdala Bin Klebu amesisitiza yakuwa hawajamtimua mwalimu huyo kwa matokeo ya mchezo wa juzi dhidi ya Simba bali kiwango cha timu hiyo kimeshuka kwasiku za karibuni. Brat's alichukua nafasi ya Tom Sentifity na sasa atalazimika kukusanya kila kilicho chake nakuitafuta barabara ya pugu itakompeleka uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere na hatimaye kupanda ndege atayeona inamfaa na kutua Amstadam Uholanzi palipo na makazi yake.

 

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather