Independent Television Ltd
Ismail Aden Rage amewataka wachezaji wa Simba kutokukata tamaa.

 Mwenyekiti wa timu ya soka ya Simba Ismail Aden Rage amewataka wachezaji wa timu hiyo kutokukata tamaa pamoja na kupoteza mchezo dhidi ya Mgambo ya mkoani Tanga.

Ismail Aden Rage mmoja kati ya viongozi wa soka anayeelekea kushabihiana kilugha  na aliyekuwa waziri wa habari ya Iraq enzi za utawala wa Sadam Hussein Ally-Sahaf amekutana na wachezaji wake hii leo baada ya kupata kizunguzungu cha kipigo cha jeshi la mgambo ya kabuku mkoani Tanga cha bao moya kwa 0.

Baada ya kipigo hicho kulikuwa na taarifa zisizo rasmi yakuwa wachezaji hawajalipwa na wengine wakipienyeza mwalimu Logarusic amekuwa mkali mno na mwenye kuwatolea wachezaji maneno yasovikwa nguo. Ismail amekana nakuwapa kongole wachezaji wake huku akasema Mgambo walijihami mno kwakurudi nyuma baada yakubahatisha goli.

Simba ilazamika kusafiri tena kuelekea mkoani Mbeya kukabiliana na walimbukaji wa ligi Mbeya city siku ya Jumamosi katika uwanja wa sokoine.

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather