Back to top

"TUMIENI UZOEFU KUHARAKISHA MABADILIKO" KUSILUKA

23 April 2024
Share

Mabalozi wamehimizwa kutumia taaluma, uzoefu na ujuzi tofauti waliokuwa nao, kuharakisha mabadiliko ya kimfumo yanayoendelea ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt.Moses Kusiluka, wakati anaongea na Mabalozi katika warsha ya siku 4 ya kutathimini utekelezaji wa Sera ya Mambo ya nje inayofanyika mjini Kibaha tokea tarehe 21 Aprili 2024..

Balozi Kusiluka amesema Serikali inazitambua changamoto wanazokabiliana nazo na inazifanyia kazi lakini kutokana na Wizara kuwa na watu wenye uzoefu wa kutoka sekta tofauti, wakishirikiana wanaweza kuzitatua na kuifikisha nchi katika hatua nzuri.
 
Balozi Kusiluka alimazia kwa kuwapongeza Mabalozi kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwaahidi kuwa Serikali itapokea mawazo yote mazuri na ya kibunifu na kuyafanyia kazi.