Back to top

WATAALAM SHERIA KUTOKA URUSI KUONESHA UZOEFU WA KUPAMBANA NA UHALIFU

29 April 2024
Share

Wataalam kutoka Ofisi kuu ya Waendesha Mashtaka Nchi Urusi, wamewasili hapa Nchini kwa ajili ya kushiriki katika kongamano la kitaaluma litakaofanyika tarehe 30 Aprili 2024 katika shule ya uanasheria kwa vitendo Tanzania ( Law School) Jijini Dar es Salaam.

Katika kongamano hilo Watalaam hao watatoa mada tatu ikiwa ni pamoja na kueleza namna ambavyo Wanasheria wa Shirikisho la Urusi wanavyofanya kazi, Utaalam na uzoefu wao katika kupambana na matukio ya uhalifu wa Kimataifa.

Prof. Ambrose Kessy kutoka Shule ya Sheria Tanzania (Law School), amebainisha hayo alipowapokea watalaam hao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Amesema watalaam hao watashirikiana na Watalaam kutoka Shule ya Sheria Tanzania kuongelea mambo hayo hivyo watu wote walio karibu ikiwemo Vyuo jirani na Taasisi ambazo zipo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria wanaalikwa kushiriki.

Amesema Kongamano hilo litahudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Pindi Chana, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na Viongozi wengine mbalimbali.