Back to top

“Hatuchukui fedha kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii”Serikali

16 April 2019
Share

Serikali imesema si kweli kwamba  imekuwa ikichukua fedha katika mifuko ya hifadhi ya jamii na kuzifanyia matumizi ikiwemo kukopesha taasisi au watu binafsi kama inavyodaiwa

Hayo yamesemwa na naibu waziri ofisi ya Waziri mkuu kazi,ajira na vijana Mhe.Antony Mavunde akijibu swali la mbunge wa Mbozi Pascal Haonga aliyeuliza juu ya tetesi za serikali kutumia fedha za mifuko na hivyo kushindwa kulipa wanachama wakiwemo wastaafu.

Amesema mifuko hiyo inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya bunge inayoanzisha mfuko husika inayosimamia muundo wa utawala na uwekezaji wa fedha za mfuko hivyo serikali haiwezi kuingilia uendeshaji wa mifuko hiyo

Mhe.Mavunde ameongeza mpaka February 2019 mfuko mpya wa PSSSF imeshalipa deni la wastaafu 9,971 kiasi cha shilingi bilioni 888.39 madeni iliyorithi kutoka mfuko wa PSPF.