Back to top

46 waathirika kwa kuvuta hewa yenye Sumu Dar es Salaam

22 May 2018
Share

Watu 46 wameathirika baada ya kuvuta hewa yenye Sumu kutoka kiwanda cha kutengeneza Sabuni cha ROYAL kilichopo Mabibo external  Jijini Dar Es Salaam.

Meneja Operesheni wa kiwanda hicho Bw. Ntuta  Shalanda  amesema  hewa hiyo imevuja kutokana na hitilafu kwenye  mtambo wa kuchuja  tindikali na tayari wamedhibiti tatizo na wamewachukua waathirika wote  na kuwapeleka hospitali kwa matibabu kwa garama zao. 

Mkuu wa wilaya ya Ubungo  Bw. Kisare  Makori  amefika eneo la tukio na kuagiza wananchi walioathrika  na tukio hilo wafidiwe na mazungumzo yaanze mara moja kuna namna yakuhamisha wanaoishi karibu na kiwanda ili kuepusha madhara zaidi.

Wananchi wa maeneo jirani wamekubali ushauri wa mkuu wa wilaya na kutaka uhakiki wa athari za mazingira ufanyike kujiridhisha  kama kinafuata sheria na taratibu.