Back to top

Abiria kisiwa cha Ukara walalamikia kupanda kwa gharama za usafiri.

11 October 2018
Share

Siku moja baada ya serikali kuvifungia vivuko vinne vya watu binafsi vilivyokuwa vinatoa huduma ya usafiri kati ya kisiwa cha Ukara na maeneo mengine ya wilaya ya Ukerewe, wakazi wa kisiwa hicho sasa wanalazimika kutumia nauli ya kati ya shilingi 2000 hadi shilingi 5000 kufika eneo la Bwisya ili kupanda vivuko vya serikali.

Uchunguzi wa ITV umebaini kuwa,kabla ya vivuko vya watu binafsi kupigwa marufuku na serikali, wananchi wa maeneo mbalimbali ya kisiwa cha Ukara walikuwa wakitumia gharama ya wastani wa shilingi 2000 kufika wilayani Ukerewe kwa ajili ya kujipatia mahitaji yao ya msingi.