Back to top

Afghanistan yawaachia huru wafungwa 900 wa Taliban.

27 May 2020
Share

Serikali ya Afghanistan imewaachia huru wafungwa 900 wa Taliban, kama ishara ya nia njema kufuatia uamuzi wa Taliban kusitisha mapigano.

Kulingana na ripoti ya serikali mjini Kabul, wafungwa hao 900 wa Taliban wameachiwa huru kutoka magereza mbali mbali nchini humo, sambamba na tukio la kihistoria la usitishwaji wa mapigano uliopendekezwa na wanamgambo wa Taliban, wakati wa kipindi cha kuadhimisha sikukuu ya Eid el-Fitr.

Wafungwa 600 waliachiwa kutoka gereza la wahalifu sugu la Bagram karibu na mji mkuu, Kabul, ambako bado Marekani ina kambi kubwa ya kijeshi.

Serikali ya Afghanistan ilikuwa imeahidi kuwaachia huru wataliban 2000, kama jibu lake kwa uamuzi wa Wataliban kutangaza ahueni ya vita kwa muda wa siku kusherehekea kumalizika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.