Back to top

Afisa 'TFS' aliyetumia jina la DC kwa udanganyifu aswekwa ndani Ikungi

09 November 2019
Share

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Edward Mpogolo amemsweka ndani Afisa msaidizi wa TFS Bwana Isack Tarama na Mfanyabiashara wa mazao ya misitu kutoka Arusha Bi, Rose Nariawe, aliyetumia jina lake na kisha kuamuru askari kuwasindikiza huku wakiwa wamebeba shehena ya mkaa uliovunwa bila kibali.

Mkuu huyo wa Wilaya ameiagiza TFS makao makuu kumchukulia hatua stahiki mtumishi huyo na Mfanyabiashara, huku akiitaka TAKUKURU kuwachunguza watumishi wengine wawili wa TFS kama kuna mazingira ya rushwa.