Back to top

Afrika Kusini yatambua mchango wa Tanzania kwenye harakati za Ukombozi

16 August 2019
Share

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amesema changamoto zinazoikabili nchi ya Tanzania zinalingana na Afrika Kusini, hivyo bora mataifa hayo yakashirikiana kuzitatua.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo mkoani Morogoro ambapo alimsindikiza Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa  ambaye alienda kumbukumbu za wapigania uhuru wa Afrika kusini ambao waliishi mkoani humo.

Naye Rais Ramaphosa amesema nchi yake inathamini mchango mkubwa wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa Afrika Kusini na daima itaendelea kuheshimu mchango huo.

Amesema Afrika ya kusini itashirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali hasa ya elimu ambapo baadhi ya shule za Sekondari na vyuo kati ya nchi hizo mbili zinakuwa na ushirikiano wa moja kwa moja katika sekta hiyo.