Back to top

Ahukumiwa miaka 60 jela  kwa kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi.

17 July 2020
Share

Mahakama ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 60 jela Clement Salama mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa kata ya Kasanga wilayani Kalambo kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba miaka 17 kisha kumpatia ujauzito.

Akisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo mwendesha  mashitaka wa Jeshi la Polisi  wilayani humo  Mlisho Kimbeho, amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo Aprili 2020 kisha kufikishwa  mahakamani kwa makosa mawili, la kwanza ikiwa ni kumbaka mwanafunzi na lapili ikiwa ni kumpatia ujauzito mwanafunzi  huyo.

Hata hivyo baada ya mahakama hiyo kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na kujiridhisha, mshitakiwa alikiri wazi kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani ni kijana mdogo ambaye bado ni tegemezi.

Awali akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo Ramadhan Rugemalira,  amesema mtuhumiwa alitenda kosa ambalo ni kinyume na kifungu cha sheria 130 (1) 2e na kifungu cha 131( 1) cha sheria kanuni ya adhabu kwa kumbaka mwanafunzi kisha kumpatia ujazito na kumsababishia kuto endelea na masomo yake.  Na kusema  Hivyo   mahakama inamuhukumu kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 60 jela.