Back to top

Ajinyonga kwa nyavu, ndani ya ofisi ya Mtendaji.

27 March 2020
Share

Watu wawili wamefariki dunia katika nyakati tofauti mkoani geita akiwemo Joseph Maneno mkazi wa kijiji cha Senga  akidaiwa kujinyonga kwa kutumia kipande cha nyavu ya kuvulia samaki  ndani ya  ofisi ya mtendaji wa kijiji  cha Kagu a Mkoani Geita alipokuwa akishikiliwa kwa tuhuma za wizi wa fedha na simu ya mkononi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli Lotson anasema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa kifo cha mtuhumiwa huyo kutokana na utata ulioibuka huku akiwataka watendaji wa vijiji na kata kufuata sheria katika ukamataji na usalama wa watuhumiwa.

Kamanda Mponjoli anasema tukio la pili limehusisha kifo cha Salago George kilichosababishwa na ajali ya gari ndogo mbili kugongana uso kwa uso  katika eneo la Mpomvu wakiwa  katika mwendo kasi na kusababisha majeruhi wanne ambao wanaendelea kupata matibabu katika hosipitali ya mkoa wa Geita na  Bugando.