Back to top

Akamatwa na begi likiwa na mkono wa binadamu

08 November 2022
Share

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia mwanaume, mkazi wa Kijiji cha Ngula, Kata ya Kanyere wilayani Misungwi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Joseph Mathias mkulima na mkazi wa kijiji cha Ngula, mwenye ulemavu wa ngozi ambaye aliuawa kwa kukatwa mkono, tarehe 02.11.2022, saa 23:00 Usiku akiwa nyumbani kwake. 
.
Jeshi hilo limebainisha kuwa tarehe 06.11.2022, saa 12:00 mchana, mtuhumiwa huyo alionekana katika kijiji cha Ngula, Kata ya Kanyere wilayani Misungwi, akiwa na begi lenye rangi nyeusi, ambalo lilitiliwa shaka na wananchi na mara moja wakatoa taarifa Polisi ambapo walipofika na kupekua begi hilo walikuta mkono wa binadamu ukiwa umeoza na unatoa harufu kali.