Back to top

Aliyekuwa Mwenyekiti wa FAT Muhidin Ndolanga afariki dunia.

18 September 2021
Share

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Tanzania (FAT) kwa sasa ikitambulika TFF, Alhaj Muhidin Ndolanga amefariki dunia jioni hii katika hospitali ya TMJ Dar es Salaam.
.
Rais wa TFF Wallace Karia ametoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na wanafamilia wa mpira walioguswa na msiba huo.
.
Karia amesema Marehemu Ndolanga wakati wa uhai wake alikuwa anapenda kuona mpira wa miguu unapiga hatua kwenda mbele.