Back to top

Ammy Ninje ainunua Mbao FC, timu hiyo kucheza soka la kulipwa Ulaya.

14 November 2020
Share

Aliyekuwa Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Ammy Ninje baada ya kuinunua Mbao FC amesema wachezaji wa timu hiyo watakuwa wakipata nafasi ya kucheza soka la kulipwa barani ulaya, huku yeye mwenyewe akiwa kocha wa timu hiyo.

Ammy Ninje amebainisha hayo kwenye kipindi cha Muziki na Michezo kinachorushwa na Radio One, ambapo kwa sasa kwasasa anaendelea na kazi zake nchini Uingereza. 

Ammy Ninje pia amesema timu hiyo itabaki na jina lake la Mbao FC na yeye atakuja kuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu hiyo huku akitarajia kuingia nchini wiki ijayo.