Back to top

Asasi za kiraia zakerwa na udhalilishaji wagombea wanawake.

19 October 2020
Share

Asasi za kiraia mkoani Mtwara zimelaani vitendo vya ukandazaji na udhalilishaji dhidi ya wagombea wanawake wanaogombea nafasi za uwakilishi nchini ikiwemo ubunge na udiwani katika majukwaa ya kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octobar 28 mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na asasi za kiraia zinazotetea haki za wanawake na vijana mkoani Mtwara ambao wanasema inasikitisha kuona  udhalilishaji wa wagombea Wanawake ukiendelea kufanywa katika majukwaa huku vyombo husika vikikaa kimya pasipo kukemea hilo.

Wamesema ni vyema viongozi wa vyama vya siasa wakajitokeza hadharani kukemea udhalilishaji huo ambao ni sehemu ya kumkandamiza mwanamke na kumdhalilisha kwa lengo la kumvunja nguvu ya kupambania ushindi wa nafasi aliyoiomba.

Kwa upande wao baadhi ya wagombea wanawake kutoka vyama vya upinzani wamekiri kuwapo kwa udhalilishaji huo, huku chama tawala CCM kikisema hakijapokea malalamiko kama hayo kwa wagombea wao lakini kimekemea udhalilishaji huo na kutaka vyombo husika kuchukua hatua.

Mashirika yaliyotoa tamko hilo ni pamoja na mlango wa matumaini kwa wanawake, Fawopa, Mtwangonet pamoja na Nerio.