Back to top

Asilimia tisa ya Watanzania wote wanaumwa ugonjwa wa kisukari

14 November 2018
Share

Leo ni siku ya Kisukari duniani huku Tanzania ikitajwa kuwa moja kati  ya nchi ambazo wananchi wake  wengi wanaumwa ugonjwa huo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh.Ummy Mwalimu amesema hayo bungeni mkoani Dodoma kabla ya kujibu maswali ambayo yalielekezwa.

Amesema mpaka sasa asilimia tisa ya Watanzania wote wanaumwa ugonjwa wa kisukari hivyo ni bora wakazingatia kanuni za afya ili wasipate madhara zaidi kutokana na ugonjwa.

Waziri Ummy Mwalimu amesema ipo haja kwa watu ambao hawana ugonjwa nao kujiepusha kwa kuzingatia kanuni za afya.