Back to top

ATCL kuanza safari kwenda China.

12 April 2019
Share

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Prof Palamagamba Kabudi amesema shirika la ndege nchini ATCL linatarajia kuanza safari za ndege ya moja kwa moja kutoka Dar es  Salaam mpaka kwenye jiji la Guangzhou nchini China ili kuchochea biashara na utalii kati ya Tanzania na China.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ofisi ndogo za ubalozi wa China jijini Dodoma Waziri Kabudi anasema Guangzhou ndio kitovu cha biashara baina ya nchi hizi mbili na safari hizo zinatarajiwa kuana kati ya mwezi June na Septemba ambapo pia mwaka ujao wa fedha Tanzania itafungua ubalozi mdogo kwenye jiji hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya mambo ya nje ulinzi na usalama Mhe Mussa Azan anasema mataifa ya Tanzania na China yana uhusiano wa kihistoria kwa muda mrefu huku balozi wa china nchini Wang ke akisema nchi yake itaendelea kuunga mkono juhudi za Tanzania kwenye mambo mbalimbali ya maendeleo.