Back to top

Athari za kimbunga zaanza kuonekana New Bern Carolina Kaskazini.

14 September 2018
Share

Watu 150,000 nchini Marekani katika majimbo ya Carolina Kusini na Kaskazini na Jimbo la Virginia hawana nishati ya umeme kufuatia upepo mkali unaovuma kutokea ukanda wa Pwani unaoelezwa kusababishwa na kimbunga kilichopewa jina la Florence.

Taarifa zinasema tayari maafa ya mafuriko yameanza kuonekana eneo la  New Bern,Carolina Kaskazini.

Kimbunga hicho kinatarajiwa pia kuyakumba maeneo ya Ufilipino na Hong Kong ambako tayari madhara ya upepo huo yameshaanza kuonekana.