Back to top

Auawa baada ya kuvamia duka na kujeruhi  watu wawili kwa risasi.

13 August 2020
Share

Jeshi la polisi mkoani Geita limemuua kwa kumpiga risasi bwana Daniel Jackson katika majibizano ya risasi,  ni baada ya mtu huyo kuvamia duka la kutoa huduma za kifedha mtaa wa Msalala kata ya Kalangalala  akiwa na bunduki aina ya Short Gun yenye risasi sita na kujeruhi watu wawili kwa kuwapiga risasi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mtatiro Kitinkwi anasema mtu huyo  alifika kwenye duka hilo majira ya jioni na kuwashambulia baadhi ya wananchi katika duka hilo ndipo kwa lengo la kupora fedha ndipo  Jeshi la Polisi likafika katika eneo la tukio na kukabiliana na mtu huyo. 

Wananchi walioshuhudia tukio hilo wamelipongeza jeshi la polisi kwa kufika eneo la tukio haraka na kuzuia uporaji pamoja na kuepusha watu wengine kujeruhiwa kwa kupigwa risasi.