Back to top

Auawa kwa kuchomwa moto baada ya kumuua mtoto wa dada yake.

27 May 2020
Share

Wananchi  wa kijiji cha Mbuluma wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamemuua kwa  mchoma moto Amosi Kapufi miaka 22 mkazi wa kijiji cha Myunga Kwa kile kilichodaiwa kumchoma kisu mtoto wa dada yake aliyefahamika kwa jina la Catherin Kakusu na  kufariki dunia papo hapo.


Vilio na huzuni kubwa imetanda kwa wakazi  wa kijiji cha Myunga baada ya kumpoteza kijana wao Amos Kapufi baada ya  kupigwa kisha kuchomwa moto na wananchi baada ya kudaiwa  kusababisha kifo cha binti Catherin Kakusu mkazi wa Mbuluma kutokana na wivu wa kimapenzi .


Mkuu  wa  wilaya ya Kalambo Julieth Binyura amethibitisha kutokea tukio hilo na kuwasihi wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.


Hata hivyo inadawa kuwa  kijana huyo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti huyo  na baada ya kutofautiana aliamua  kuchoma na kisu katika sehemu za tumbo na kifuani na kusababisha kifo cha binti huyo.